VENEZUELA-SIASA

Bunge la Katiba la Venezuela lapitisha sheria dhidi ya chuki, upinzani walalama

Upinzani unaona sheria hii kuwa ni tishio dhidi ya chama chochote kinachompinga Nicolas Maduro.
Upinzani unaona sheria hii kuwa ni tishio dhidi ya chama chochote kinachompinga Nicolas Maduro. Palacio de Miraflores

Nchini Venezuela, Bunge la Katiba, linaloundwa na tu wafuasi wa rais Nicolas Maduro, liliidhinishwa siku ya Jumatano, Novemba 9, "sheria dhidi ya chuki, kwa msikamano wa amani na uvumilivu.

Matangazo ya kibiashara

" Sheria hii, iliyopendekezwa kwa Bunge la Katiba na rais Maduro mwezi Agosti mwaka huu, imechapishwa gazeti la serikali. lSheria hii imetoa adhabu ya miaka ishirini jela dhidi ya watu watakaopatikana na hatia ya "uhalifu na uhalifu".

Serikali ya Venezuela inasema kuwa sheria hii itauzuia vurugu nchini humo; upinzani unaona kinyume chake kitendo cha kusambaratisha amani, hali ambayo ni "hatari kwa uhuru wa kujieleza" nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa nakala hii iliopigiwa kura na Bunge la Katiba, hukumu zinaweza kuwahusisha watu, lakini pia vyama vya siasa. Vyama vya siasa vinaweza kuondolewa kutoka kwa halmashauri ya kiaifa ya Uchaguzi na hivyo kuchukuliwa kama havifuatishi sheria ikiwa havitaheshimu sheria.

Na vikwazo vinaweza pia kutumika dhidi ya vyombo vya habari ikiwa haviheshimu sheria hii, kuanzia faini hadi kufungwa.

Mbunge Tamara Adrian anaona tishio dhidi ya chama chochote kinachompinga Nicolas Maduro, kuanzia kwa Voluntad Popular, chama cha mwanasiasa wa upinzani aliyewekwa chini ya kifungo cha nyumbani, Leopoldo Lopez.

Sheria hii ni "chombo cha kuzuia uhuru wa kujieleza", wamesema wanaharakati wa haki za binadamu nchini Venezuela. Hii pia ni kile Marekani ilishtumu siku ya Alhamisi ikizungumzia juu ya sheria hii baada ya kuweka vikwazo vipya vya kifedha dhidi ya viongozi kumi wa Venezuela.