MAREKANI-URUSI

Trump awashukia wakosoaji wa juhudi zake kuimarisha uhusiano na Urusi

Rais wa Marekani Donald  Trump akiteta jambo na rais wa Urusi  Vladimir Putin kabla ya mkutano wa APEC huko Danang, Vietnam Novemba 11, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump akiteta jambo na rais wa Urusi Vladimir Putin kabla ya mkutano wa APEC huko Danang, Vietnam Novemba 11, 2017. Sputnik/Mikhail Klimentyev/Kremlin

Rais wa Marekani Donald leo Jumapili ameshusha dhoruba ya jumbe kwenye ukurasa wake wa twitter kwa wale aliowaita wapinzani na wapumbavu wanao hoji kuhusu juhudi zake za kuboresha uhusiano na Urusi na kuelekeza zaidi ujumbe wake kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Kong-Un.

Matangazo ya kibiashara

Trump ameandika kuwa ni lini wenye chuki na wapumbavu watatambua kuwa kuwa na uhusiano mzuri na Urusi ni jambozuri na si baya?na kwamba anataka kutatua mgogoro wa Korea Kaskazini, Syria , Ukraine na ugaidi na Urusi inaweza kusaidia.

Rais Trump ambaye kwa sasa yuko Vietnam akielekea ukingoni mwa ziara yake katika mataifa matano ya ukanda, amekuwa kimya katika mtandao wa Twitter tangu alipoondoka Washington,hii leo ametuma jumbe kadhaa mfululizo kabla ya sherehe ya mapokezi yake rasmi huko Hanoi.