MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Waziri wa Sheria wa Marekani aitishwa bungeni

Waziri wa Sheria wa Marekani Jeff mbele ya bunge la Seneti, Juni 13, 2017.
Waziri wa Sheria wa Marekani Jeff mbele ya bunge la Seneti, Juni 13, 2017. SAUL LOEB / AFP

Waziri wa Sheria wa Marekani Jeff Sessions anatazamia kushuhudia mbele ya bunge la Wawakilishi Jumanne hii, Novemba 14, kuhusu Urusi kuingilia katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya bunge la Seneti mwezi Juni, Jeff Sessions alijaribu kujitetea. "Kwa uwelewa wangu sijawahi kuwasiliana na Urusi kuhusu uchaguzi wa urais wa Marekani," Bw. Sessions amesema. Jeff Sessions ambaye alikua kiongozi wa timu ya washauri wa Donald Trump kuhusu sera yake ya kigeni wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais, alihojiwa wakati huo kuhusu mawasiliano kati ya timu ya mgombea wa chama cha Republican na maafisa wa Urusi.

Lakini taarifa ya Waziri wa Sheria wa Marekani ilikanushwa na George Papadopoulos, mshauri wa zamani wa kampeni wa Donald Trump kuhusu mambo ya kigeni. Katika ushuhuda wake kwa polisi wa Marekani, Bw. Papadopoulos alihakikisha kwamba alikua na uhusiano maalum na Urusi katika mkutano wa Machi 2016, ambapo Jeff Sessions alishiriki.

Ushahidi mwingine unaweza kumuweka hatarini Waziri wa Sheria wa Marekani. Mbele ya Kamati ya upelelezi ya bunge la Wawakilishi wiki mbili zilizopita, Page Carter, pia mshauri wa kampeni wa rais wa Donald Trump, alisema alikwenda kwa ziara isio rasmi mjini Moscow kabla ya uchaguzi wa urais, na alikua na mawasiliano "mafupi" na Naibu Waziri Mkuu wa Urusi. Alisema alimuonya Jeff Sessions kwa ziara yake hiyo.

Jeff Sessions atajieleza kuhusu shutma hizi mbili mbele ya bunge la Seneti. Wabunge kutoka chama cha Democrat wamesema watataka kujua ukweli kuhusu hali hiyo.

Kwa mujibu wa baadhi ya waangalizi, Jeff Sessions anakabiliwa na kibarua kigumu na huenda hatma yake ikawa mbaya.