ARGENTINA-AJALI-USALAMA

Argentina yakata tamaa kuipata manowari yake iliyozama

Kambi ya kikosi cha wanamaji ya Mar del Plata, bandari ambapo manowari ya San Juan, ilianzia safari yake kabla ya kupata ajali, 18 Novemba 2017.
Kambi ya kikosi cha wanamaji ya Mar del Plata, bandari ambapo manowari ya San Juan, ilianzia safari yake kabla ya kupata ajali, 18 Novemba 2017. REUTERS/Marcos Brindicci

Serikali ya argentina imesem ahakuna matumaini ya kuwapata hai askari wa kikosi cha wanamaji waliokua wakisafiri na manowari ya Argentina ya San Juan ambayo inadaiwa kuwa ilizama baada ya kutokea mlipuko.

Matangazo ya kibiashara

Utafiti unaendelea wa kuipata manowari hiyo, huku familia za wanamaji hao wakiwa tayari wamekata taama ya kuwapata hai ndugu zao.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Buenos Aires siku ya Alhamisi, msemaji wa kikosi cha wanamaji cha Argentina, Kapteni Enrique Baldi alitangaza kuwa tathmini iliyotolewa na Austria ilibaini kwamba kulitokea mlipuko ndani ya manowari hiyo kabla ya kuzama.

Mamlaka ya Argentina na meli na ndege za kigeni zinaendelea kujaribu kupata manowari hiyo katika bahari ya kusini mwa Atlantic. Taarifa ya mwisho iliotolewa ilibaini kuwa maonowari hiyo ilikuwa kilomita 400 kutoka pwani ya Argentina ya Patagonia.

Tangu siku ya Jumatano jioni, meli tatu zinasafiri eneo ambapo mlipuko ulitokea, ambapo kina cha urefu kiko kati ya mita 200 hadi 3,000. Chini ya mita 600, manowari ya San Juan ingelifaulu kutoka, kwa mujibu wa wataalam.

- Jitihada za Kimataifa -

Zaidi ya watu 4,000, meli kumi na nne na ndege kumi zinaendelea kutafuta manowari hiyo, kwa msaada wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Brazil na Chile. "Jitihada za kitaifa na kimataifa zenye uwezo mkubwa zinaendelea", kwa mujibu wa kikosi cha wanamaji cha Argentina.