MAREKANI-UISLAMU-HAKI

Donald Trump asambaza kwenye Twitter video dhidi ya Waislam

Rais wa Marekani Donald Trump aendelea kukosolewa duniani kwa msimamo wake dhidi ya raia kutoa nchi zenye Waislamu wengi.
Rais wa Marekani Donald Trump aendelea kukosolewa duniani kwa msimamo wake dhidi ya raia kutoa nchi zenye Waislamu wengi. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump amejiunga kwenye Twitter ya video tatu dhidi ya Waislamu iliorushwa mitandaoni na chama kidogo cha mrengo wa kulia nchini Uingereza, "Britain First".

Matangazo ya kibiashara

Wakati alipokua mgombea wa chama cha Republican, Trump alitetea hoja yake ya kupiga marufuku kuingia nchini Marekani wageni kutoka nchi za Kiislamu, na baada ya kuwa rais alitoa agizo inayopiga marufuku kuingia nchini Marekani raia kutoka nchi kadhaa zenye Waislamu wengi, ingawa mahakama zilizuia marufuku hiyo kuanza kutumika.

Jayda Fransen, kiongozi wa chama cha " Britain First", ambae alirusha video hizo kwenye Twitter leo Jumatano, akisema kuwa video hizo, moja imekua ikionyesha kundi la Waislamu wakimpiga hadi kufariki kijana mmoja, na video nyingine inaonyesha kijana mlemavu akisahambuliwa na video ya tatu ikionyesha watu wakiharibu sanamu ya Kikristo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ambalo halijaweza kuthibitisha uhalisi wa video hizo, Donald Trump mwenyewe amejiunga kwa video hizo na ana marafiki kwenye Twitter wanaokaribia milioni 44.

"Mungu akubariki, Trump!", Britain First imeandika, ambapo akaunti yake ya Twitter ina jumla ya marafiki 24,000.

"Ninafurahi," Jayda Fransen ameliambia shirika la habari la Reuters. Ujumbe muhimu kwa sisi ni kwamba Donald Trump anajua mateso na mashtaka ya mwanasiasa wa Uingereza alieshtumiwa kufanya kile ambacho polisi inachukulia kama hotuba dhidi ya Waislam "Jayda Fransen amesema.

Jayda Fransen alitozwa faini mwezi huu baada ya kupatikana na hatia ya unyanyasaji mkubwa wa kidini, kwa kumdhalilisha mwanamke wa Kiislamu aliyevaa hijab.

Wiki iliyopita, alihukumiwa na polisi ya Ireland ya Kaskazini kwa kutoa maneno kama vitisho au matusi wakati alipokua akihotubia umati wa watu mwezi Agosti mjini Belfast.