UINGEREZA-MAREKANI-UISLAM-HAKI

Theresa May amshtumu Trump kusambaza vedeo ya chuki dhidi ya Uislam

Waziri Mkuu wa uingereza Theresa May ameendelea kumlaumu rais wa Marekani Donald trump kuchochea chuki dhidi ya Uislam..
Waziri Mkuu wa uingereza Theresa May ameendelea kumlaumu rais wa Marekani Donald trump kuchochea chuki dhidi ya Uislam.. REUTERS/Maurizio Degl'Innocenti

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema Rais wa Marekani Donald Trump alifanya Makosa kuisambaza video ya chuki dhidi ya Uislam kupitia mtandao wake wa Twittter.

Matangazo ya kibiashara

Theresa May anasema licha ya kumkosoa kiongozi huyo kwa kusambaza video inayoeneza chuki dhidi ya uislam lakini mahusiano baina na Uingereza na Marekani yataendelea

Awali May alimlaumu Trump kwa kumshambulia kwa maneno ambapo katika mtandao wa Twitter Trump aliandika kuwa "May asijikite kuhusu mimi, jikite katika ugaidi wa kiislam unatokea nchini Uingereza."

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akielekea Jordan Waziri Mkuu wa Uingereza ametetea historia aliyonayo kuhusu kusimamia ubaguzi wa kidini ikiwa ni pamoja na kusimamia haki huku akihamasisha, mahusiano ya nchi hizo mbili kuendelea.

Wakati huo huo Meya wa jiji la London Sadiq Khan, ambae nae amehusishwa katika mvutano huo wa Trump, amesema vitendo vya rais huyo ni usaliti wa mahusiano maalum kati ya nchi ya Marekani na Uingereza.