BRAZIL-RUSHWA-HAKI

Uamuzi kuhusu rufaa ya Lula kutolewa Januari 24 Brazil

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anakabiliwa na kifungo cha miaka 10.
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anakabiliwa na kifungo cha miaka 10. REUTERS/Fernando Donasci

Mahakama ya Brazil itatoa uamuzi wake juu ya rufaa ya rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva Januari 24, 2018. Rais huyo wa zamani wa Brazil alihukumiwa baada ya kupatikana na hati ya kashfa ya rushwa, ambayo inaweza kumzuia kuwania katika uchaguzi wa urais ambao ulipangwa kufanyika mwaka 2018 nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya hatia hiyo na mashtaka mengine manne ya rushwa, rais wa zamani wa Brazili, anaendelea kuwa kiongozi wa kisiasa anaependwa na wananchi wa Brazil na anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais ujao, kulingana na uchunguzi wa kwanza.

Ikiwa Kitengo cha Rufaa cha mahakama ya kikanda ya Porto Alegre kitathibitisha hukumu yake, "Lula" anaweza kukata rufaa mpya kwa mahakama za juu lakini hatokubaliwa kushiriki katika uchaguzi wa urais.

Wanasheria wa Lula, hata hivyo, wamekosoa namna uamuzi wa mahakama unaharakishwa.

Rais wa zamani, kuanzia mwaka 2003 hadi 2010, alihukumiwa mnamo mwezi Julai kifungo cha miaka 10 kwa kukubali kupokea Reals milioni 3.7 (sawa na Euro 953,000) kutoka kwa kampuni ya OAS kwa kukarabati ghorofa ilio katika eneo la Guaruja kama shukrani kwa kuingilia kati kwa kupewa mikataba na kampuni ya petroli ya Petrobras inayomilikiwa na serikali.