PERU-HAKI

Rais wa zamani wa Peru aomba msamaha, Rais Kuczynski ajieeleza

Waandamanaji wakiandamana katika mji wa Lima dhidi ya kuachiwa huru kwa rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori. Kwenye bango kumeandikwa "Fujimori muuaji", Peru, Desemba 25, 2017.
Waandamanaji wakiandamana katika mji wa Lima dhidi ya kuachiwa huru kwa rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori. Kwenye bango kumeandikwa "Fujimori muuaji", Peru, Desemba 25, 2017. REUTERS/Mariana Bazo

Kiongozi wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori, amewaomba radhi wananchi wa taifa hilo, siku mbili baada ya kupokea msamaha wa rais ambao ulisababisha maandamano mitaani kupinga hatua hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia video kwenye mtandao wa Facebook iliyorekodiwa akiwa katika kitanda cha hospitali Fujimori amesema anatambua kuwa matokeo ya serikali yake yalipokelewa vizuri kwa upande mmoja, lakini anaikubali kwamba amewaangusha wafuasi wake wengine, na anawaomba kwa dhati, wamsamehe.

Fujimori mwenye umri wa miaka 79 alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 25 kwa makosa ya rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa wakati akiwa madarakani tangu mwaka 1990 hadi 2000.

Alihamishwa kutoka gerezani hadi hospitali siku ya Jumamosi baada ya kushambuliwa na shinikizo la damu na mabadiliko ya mapigo ya moyo, katika mabadiliko ya hivi karibuni katika mfululizo wa kuugua kwake.

Mapema siku ya Jumapili rais Pedro Pablo Kuczynski aliamuru kuachiwa huru kwa Fujimori na wafungwa wengine saba kwa misingi ya kibinadamu,na kujiweka katikati ya mgogoro wa kisiasa siku chache tu baada ya kunusurika kuondolewa madarakani.