MAREKANI-TRUMP-MAJANGA ASILI

Nyumba ya Trump yawaka moto New York, wawili wajeruhiwa

Mbele ya mnara wa nyumba ya Donald Trump, Trump Tower,  New York ambapo moto ulizuka mapema Jumatatu hii asubuhi Januari 8, 2017.
Mbele ya mnara wa nyumba ya Donald Trump, Trump Tower, New York ambapo moto ulizuka mapema Jumatatu hii asubuhi Januari 8, 2017. REUTERS/Twitter/@oinonio

Moto umezuka kwenye mnara ya moja ya nyumba za rais wa Marekani Dnald trump, Trump Tower, katika mji wa New york, nchini Marekani. Moto huo umesababisha watu wawili kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mmoja aambaye yuko katika hali mbaya, maafisa wa Zima Moto wametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kisa hicho kimetokea wakti ambapo rais Trump alikuwa Washington.

Eric Trump, mmoja wa wanawe, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba moto huo ulizuka kutokana na matumizi mabaya ya umeme katika mfumo wa kuingiza baridi kwenye jengo, kupitia paa la mnara.

"Maafisa wa Zima Moto wa New York waliwasili dakika chache baada ya moto huo kuzuka na wamefanya kazi ya kushangaza," ameongeza Eric Trump. "Wanaume na wanawake wa FDNY ni mashujaa wa kweli na tunatoa shukrani zetu za dhati!".

"Moto ulizuka muda mfupi kabla ya saa 07:00 saa za Marekanii (saa sita mchana GMT) kwenye mnara wa Trump Tower wa jengo lenye ghorofa 52 linalokwenda juu mita 202.