SALVADOR-MAREKANI-USHIRIKIANO

Raia 200,000 wa Salvador waishio Marekani wakabiliwa na hali nzito

Ubalozi wa El Salvador, New York, Januari 8, 2018.
Ubalozi wa El Salvador, New York, Januari 8, 2018. REUTERS/Andrew Kelly

Utawala wa Marekani umetangaza kwamba hautarejelea upya mpango ulioanza kutekelezwa mwaka 2001 ambao umewawezesha watu 200,000 kutoka El Salvador kuishi na kufanya kazi katika ardhi ya Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Marekani umetoa hadi mwezi Septemba 2019 kwa watu hao kuondoka nchini humo. Donald Trump anaendeleza sera yake ya kuzuia wageni kuishi nchini Marekani.

Utawala wa Marekani ulichukua hatua kama hiyo kwa raia wa Haiti mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita 2017. Wizara ya Usalama nchini Mareani inasema kuwa hali ya maisha imeimarika vya kutosha katika nchi yao kwa raia wa El Salvador walikua wakinufaika kwa mpango huo kurudi nyumbani.

Marekani ilianzisha mpango huo kwa raia 200,000 wa El Salvador kufuatia tetemeko la ardhi kubwa na baya lililotokea mwaka 2001. Tangu wakati huo watoto 193,000 wa El Salvador walizaliwa nchini Marekani. Mwezi Septemba mwaka huu, wataamua kuishi kama wahamiaji haramu nchini Marekani kwa hatari ya kufukuzwa, kuondoka na familia zao au kuondoka nchini Marekani na kukabidhi watoto wao kwa watu maalumu ili waweze kuendelea kuishi nchini Marekani.

Nchi ya El Salvador imejenga upya miundombinu yake tangu kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi, lakini vurugu zimeendelea kusababisha uchumi kudorora. Kulingana na Benki ya Dunia, familia nne kati ya kumi zinaishi chini ya kiwango cha umasikini. Zaidi ya dola bilioni 4.5 hutumwa kila mwaka kwa nchini humo kutoka raia wa nchi hiyo waishiyo nje, hasa nchini Marekani

Na hata kama wataamua kuishi nchini Marekani kinyume cha heria, wengi wa watapoteza kazi zao kwenye.