MAREKANI-TRUMP-HAKI

Trump kuhojiwa kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani

Mkuu wa zamani wa FBI Robert Mueller, mnamo 21 Juni 2017, ni mwendesha mashitaka anayehusika na kuchunguza uwezekano wa Urusi kuingilia katika kampeni ya uchaguzi wa urais ya Donald Trump.
Mkuu wa zamani wa FBI Robert Mueller, mnamo 21 Juni 2017, ni mwendesha mashitaka anayehusika na kuchunguza uwezekano wa Urusi kuingilia katika kampeni ya uchaguzi wa urais ya Donald Trump. Alex Wong/Getty Images/AFP

Mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump wanashauriana na wachunguzi wanaotarajia kumhoji Trump, kuhusu anachokifahamu kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.

Matangazo ya kibiashara

Robert Mueller anayeongoza uchunguzi huo, anatarajiwa kumhoji rais Trump hivi karibuni.

Rais Trump na wale wote waliomsaidia kipindi cha kampeni wameendelea kukanusha madai kuwa walishirikiana na Urusi, kumsaidia kushinda urais.

Urusi pia imekanusha madai hayo. Lakini washirika wa karibu wa zamani wa Donald Trump wameendelea kuhakikisha kuwa kulikuepo na mikutano iliyofanyika mara kadhaa kati ya maafisa wa Urusi na ndugu na washirika wa karibu wa Bw Trump.

Alipoulizwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita kuhusukuhojiwa kwake, Donald trump alijibu kwamba hatoficha chochote kile. Donald Trump anataka kukamiliza uchunguzi ambao umeendelea kuharibu muhula wake, ambapo anaona kuwa ni aibu kwa Marekani.

Lakini wanasheria wake wameshtumu kuona mteja wao atakutana uso kwa uso na Robert Mueller anayeongoza uchunguzi huo, wamekua wakijaribu Madai ambayo yamefutiliwa mbali na timu ya mwendesha mashitaka.

Haitakuwa mara ya kwanza rais kuhojiwa na mahakama akiwa madarakani. Bill Clinton alitakiwa kujieleza kuhusu tuhuma za ngono katika kesi ya Lewinsky na George Bush alihojiwa katika ofisi ya mashitaka kuhusu kutoa utambulisho wa afisa wa shirika la ujasusi la CIA.