MAREKANI-TRUMP-WAHAMIAJI

Donald Trump aendelea kujitetea kuhusu kauli yake bungeni

Rais wa Marekani Donald Trump  anasema hajawahi kuwa mbaguzi na kusisitiza kuwa, hajawahi kufikiria kufanya hivyo.
Rais wa Marekani Donald Trump anasema hajawahi kuwa mbaguzi na kusisitiza kuwa, hajawahi kufikiria kufanya hivyo. REUTERS/Joshua Rob

Rais wa Marekani kwa mara nyingine, amesema alieleweka vibaya baada ya kutumia neno shimo la choo, kuelezea mataifa ya Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Trump amesema, madai hayo yanarejesha nyuma juhudi za kufikia mwafaka wa kuwatambua na kuwasaidia wahamiaji walio na nia njema wanaokwenda Marekani.

Aidha, amemshutumu Seneta wa chama cha upinzani cha Democratic Dick Durbin kwa kuanza kusambaza habari za uongo kuwa alikuwa ametumia lugha ya kibaguzi alipokutana na wabunge kujadilia masuala ya wahamiaji.

Rais wa Marekani ameendelea kukosolewa ulimwenguni kwa kutumia lugha mbaya na hatua zake ambazo zinaonekana kuwatenga baadhi ya raia kutoka mataifa mbalimbali.

Wadadisi wanasema Donald Trump ni rais wa kwanza wa Marekani, ambaye kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja hatua zake zimepata upinzani mkubwa na hata kufutiliwa mbali katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo.