MAREKANI-UHAMIAJI-USALAMA

John Kelly: Trump hakua na taarifa kuhusu suala la uhamiaji

Mkuu wa Utumishi wa Umma nchini Marekani John Kelly amewaambia wabunge wa upinzani wa chama cha Democratic kuwa, rais Donald Trump hakuwa na taarifa za kutosha kuhusu baadhi ya matamshi na maamuzi kuhusu suala la wahamiaji nchini humo.

Donald Trump na Jenerali Mstaafu John Kelly (kulia), Novemba 20, 2016.
Donald Trump na Jenerali Mstaafu John Kelly (kulia), Novemba 20, 2016. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Aidha, amesema matamshi ya Trump kuwa atajenga ukuta kati ya Marekani na Mexico, ni kauli ambayo Kelly amesema Trump aliitoa bila ya kufahamu undani wake.

Hivi karibuni Rais Trump alitumia neno shimo la choo, kuelezea mataifa ya Afrika. Lakini alijirudi na kusem akuwa alieleweka vibaya, na hivyo kumshtumu Seneta wa chama cha upinzani cha Democratic Dick Durbin kwa kuanza kusambaza habari za uongo kuwa alikuwa ametumia lugha ya kibaguzi alipokutana na wabunge kujadilia masuala ya wahamiaji.

Rais Trump amekuwa akikosolewa kwa kufanya maamuzi na kutoa kauli ambazo zimeendelea kuonekana kupoteza maadili ya taifa la Marekani hasa, suala la kuwapa hifadhi wahamiaji.

Wadadisi wanasema Donald Trump ni rais wa kwanza wa Marekani, ambaye kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja hatua zake zimepata upinzani mkubwa na hata kufutiliwa mbali katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo.