BRAZIL-RUSHWA-HAKI

Hatma ya rais wa zamani wa Brazil kujulikana Jumatano hii Brazil

Hatima ya Lula iko mikononi mwa mahakimu watatu (picha ya zamani).
Hatima ya Lula iko mikononi mwa mahakimu watatu (picha ya zamani). REUTERS/Leonardo Benassatto

Mahakama ya Rufaa nchini Brazili inatazamiwa kutoa uamuzi wake leo Jumatano Januari 24 kuhusu kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva. Idadi kubwa ya polisi imetumwa katika mji wa Porto Alegre, kusini mwa Brazil, ambapo uamuzo huo utatolewa.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya mwanzo ilimuhukumu Bw Lula kifungo cha miaka 9 na nusu jela, baada ya kupatikana na hatia ya rushwa.

Lula hatahudhuria kesi yake. Lakini alikuja jana Jumanne jioni kukutana na maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika karibu na mahakama ya Porto Alegre.

Wafuasi wake wanaomba rais huyo wa zamani, anayetaka kuwania tena kiti cha urais mnamo mwezi Oktoba, aachiwe huru.

Bila kuingia katika maelezo ya kisheria, Lula alituma hasa ujumbe wa kisiasa wa ulinzi wa uhuru wa taifa na ushirikiano wa Amerika ya Kusini.

Hatima ya Lula iko mikononi mwa mahakimu watatu. Wanatarajia kuamua ikiwa alipokea hongo kama sehemu ya kashfa ya rushwa kutoka Petrobras, kampuni ya mafuta ya serikali.

Hukumu hii sio ya mwisho. Kuna uwezekano wa kukata rufaa kwa pande zote mbili. Lakini kesi hii inafanyika katika ya sitntofahamu, kwa sababu Lula mwanasiasa maarufu nchini Brazil.