MAREKANI-URUSI-UCHAGUZI-SIASA

Tillerson aionya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson.
Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson. REUTERS/Alex Brandon/Pool

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Urusi itakiona cha mtema kuni iwapo itaingilia Uchaguzi wa wabunge, utakaofanyika mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

ayari Mkurugenzi wa Shirika la Inteljensia la CIA Mike Pompeo amesema kuwa, anatarajia Urusi kujaribu kuingilia Uchaguzi huo kama inavyoaminika kuwa, mwaka 2016 iliingilia uchaguzi wa urais na kumsaidia rais Donald Trump kushinda.

Hata hivyo, Urusi imeendelea kukanusha madai ya kuingilia siasa za Marekani licha ya uchunguzi unaendelea kwa sasa kubaini iwapo kuna ukweli huo.

Aliyekua mgombe katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton aliishtumu Urusi kusababisha anashindwa katikia uchaguzi huo.

Bi Clintn alisem alishindwa kufuatia Urusi kuingilia uchaguzi huo.