MAREKANI-TRUMP-HAKI

Mwanasheria wa Donald Trump adai kutolipwa fedha zake

Mwanasheria wa Donald Trump, Michael Cohen, anasema mteja wake hajamlipa fedha zake alizotoa kama malipo kwa Stormy Daniels.
Mwanasheria wa Donald Trump, Michael Cohen, anasema mteja wake hajamlipa fedha zake alizotoa kama malipo kwa Stormy Daniels. REUTERS/Yuri Gripas

Mwanasheria wa Donald Trump amekiri kulipa dola130,000 kutoka mfuko wake kwa mwigizaji wa filamu nchini Marekani, Stephanie Clifford, anayejulikana kwa jina la Stormy Daniels, ambaye anasema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotumwa kwa gazeti la New York Times, ambalo liliifichua jana Jumanne, Februari 13, Michael Cohen anakubali kuwa amelipa dola 130,000 (sawa na euro 100,000) kwa nyota wa filamu za Marekani Stormy Daniels, mwaka 2016, wakati wa kampeni ya uchaguzi wa urais, madai ambayo yalifichuliwa na gazeti la Wall Street Journal mnamo mwezi Januari.

Hata hivyo Bw Cohen hakuelezea sababu ya malipo haya, ambayo ametaja kuwa yalikua malipo halali.

Michael Cohen amehakikisha kuwa hakuweza kulipwa na kundi la kampeni ya Donald Trump. Stormy Daniels anadai kuwa alikuwa na uhusiano a kimapenzi na Donald Trump mnamo mwaka 2006.

Wakati huo huo ikulu ya Whit House imekanusha madai hayo, ikisem akuwa ni upuuzi mtupu.

"Hakuna kampuni hata moja ya Bw Trump wala kundi la kampeni la Trump lililofikia mkataba wa malipo na Bibi Clifford, wala hakuna hata mmoja wao alinipa malipo haya, moja kwa moja au kupitia mtu mwengine," amesema mwanasheria, akinukuliwa na gazeti la kila siku la Wall Street Journal. "Malipo kwa Bibi Clifford yalikuwa halali na haikuwa mchango kwa kampeni au kwa gharama za kampeni ya mtu yeyote." Gazeti la Wall Street Journal linasema kuwa malipo hayo yalikuwa ya kununua haki miliki ya mwigizaji huyo muda mfupi kabla ya uchaguzi wa urais.

Stephanie Clifford, amesema alitembea kimapenzi na Donald Trump mnamo mwezi Julai 2006, wakati wa mashindano ya golf, wakati ambapo bilionea huyo alikuwa tayari ameshaoa.