MAREKANI-STORMY-HAKI

Stormy Daniels atishia kuweka hadharani uhusiano wa kimapenzi na Trump

Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006.
Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006. AFP

Muigizaji nguli wa filamu nchini Marekani Stephanie Clifford anayejulikana kwa jina la Stormy Daniels ametishia kuweka hadharani uhusiano wake wa kimapenzi na rais wa sasa wa Marekani Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Stephanie Clifford amesema mwanasheria wa Donald Trump alimkubalia kuwa makubaliano yao ni ya siri.

Mwakilishi wa Stormy Daniels ameviambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba mteja wake hakuwahi kulazimishwa makubaliano hayo, kwa kuwa kuwepo kwa makubaliano hayo ilithibitishwa na mwanasheria wa Rais Donald Trump, Michael Cohen. "Stormy ataelezea historia yake," Mwakilishi wa Stormy Daniels amesema.

Habari hii ilianza kugonga vichwa habari Januari 12, wakati gazeti la Wall Street Journal lilidai kwamba Stephanie Clifford, mwenye umri wa miaka 38, anayejulikana kama Stormy Daniels, alilipwa ili kutofichua siri kuhusu kutembea kimapenzi na Donald Trump wakati ambapo alikua tayarialimuoa Melania, mke wa sasa wa rais Donald Trump. Uhusiano huu wa kimapenzi ulifanyika mnamo mwaka 2006, miezi minne baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao Barron.

Ikulu ya White House imekua ikikanusha madai haya, iliyoyataja kama "habari za zamani zilizorekebishwa, kuchapishwa na kukanushwa kabla ya uchaguzi".

Mapema wiki hii mwanasheria binafsi wa Donald Trump alithibitisha kwamba makubaliano na mwigizaji Daniels yalifikiwa lakini kwamba alimlipa kwa fedha zake.