MAREKANI-USALAMA

Kruz akiri kuwaua wanafunzi katika shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas

Nicholas Kruz alikamatwa na polisi katika eneo hili baada ya kuwaua kwa risasi wanafunzi, Februari 14, 2018.
Nicholas Kruz alikamatwa na polisi katika eneo hili baada ya kuwaua kwa risasi wanafunzi, Februari 14, 2018. WSVN.com via REUTERS

Nicholas Kruz , kijana mwenye umri wa miaka 19 amekiri kutekeleza shambulio na kuwaua wanafunzi wa shule moja Mjini Florida huku shirika la ujasusi la Marekani FBI ikikiri kushindwa kuzuia shambulio hilo licha ya kuarifiwa mapema

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Marekani inashuhudia shambulio baya la risasi kwa wanafunzi wa shule tangu lilipotokea shambulio lingine miaka sita iliyopita katika shule ya Sand Hook miaka sita iliyopita.

Shambulizi la wanafunzi wa shule ya Wanafunzi wa shule ya Marjory Stoneman Douglas High School iliyopo Parkland limetokea jana ambapo licha ya kuomba msaada na kujificha chini ya madawati walishambuliwa na Nikolas Cruz aliyekuwa na risasi aina ya AR-15

Rais Donald Trump ameeleza chanzo cha matukio hayo kuwa ni matatizo ya akili na kukwepa kuzungumzia suala la umiliki wa silaha.

Ameshatkiwa kwa makosa 17 yakiwemo ya mauaji ya kupangwa ambapo jaji anayeendesha kesi hiyo ameamuru aendelee kushikiliwa.