VENEZUELA-PERU-USHIRIKIANO

Mvutano waibuka kati ya Peru na venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika mkutano na waandishi wa habari Februari 15, Caracas.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika mkutano na waandishi wa habari Februari 15, Caracas. REUTERS/Marco Bello

Mvutano umejitokeza kuelekea mkutano wa kilele wa nchi za Amerika utakaofanyika katika mji mkuu wa Peru, Lima mnamo mwezi Aprili. Mkutano huo utajumuisha viongozi wa nchi 35 za bara la Amerika mnamo tarehe 13 na 14 Aprili.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo mamlaka nchini Peru imesema haitaki kuona rais wa Venezuela Nicolas Maduro anahudhuria mkutano huu.

Hata hivyo, siku ya Alhamisi Nicolas Maduro alihakikisha kwamba atakwenda Lima kwa mkutano ujao.

Rais Maduro alisema akijibu serikali ya Peru kwamba lazima atahudhuria mkutano wa kilelea wa nchi za Amerika.

"Je, wananiogopa? Hawataki kuniona huko Lima? Wataniona! watake wasitaki, nitakwenda kwenye mkutano wa nchi za Amerika ili kutoa ukweli wa Venezuela! " alisema Nicolas Maduro, ambaye anatarajia kuhudhuria mkutano uliopangwa kufanyika zikisalia siku zisizozidi 10 kabla ya uchaguzi wa urais nchini Venezuela.

Rais Maduro ameendelea kutengwa kimataifa kufuatia visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea katika nchi yake.

Hata hivyo Cuba imeendelea kumuunga mkono Rais Nicolas Maduro.