MAREKANI-USALAMA

Trump: Nasikitishwa na muda uliotumiwa na FBI kuchunguza Urusi

Donald Trump alishtumu shirika la ujasusi la FBI kupuuzia tahadhari za usalama katika shule ya Parkland, Florida.
Donald Trump alishtumu shirika la ujasusi la FBI kupuuzia tahadhari za usalama katika shule ya Parkland, Florida. REUTERS/Eric Thayer

Rais Donald Trump amelishtumu shirika la ujasusi la FBI kupuuza ishara za tahadhari ambazo zingeliweza kuzuia mauaji katika shule ya Highland ya Parkland na kujihusisha tu na uchunguzi kuhusu Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Bw Trump amesema kuwa FBI haikutoa ushahidi wowote kutokana na na hali hiyo kwa kuhusiana na kesi hizo mbili.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akibaini kwamba Urusi ilikuwa ilifikia lengo lake la kuchochea "ugomvi, ghasia na machafuko nchini Marekani". "Walicheka sana mjini Moscow," alisema Bw Trump katika mfululuzi wa jumbe zake hizo kwenye Twitter kutoka makazi yake huko Mar-a-Lago, Florida.

Kauli hii ya Rais Trump inakuja siku mbili baada ya Mwendesha Mashitaka maalum Robert Mueller kuwahukumu Wamarekani 13 na makampuni matatu ya Urusi, kuingilia uchaguzi Marekani

Alishutumu pia mtangulizi wake Barack Obama ambaye hakuchukua hatua za kutosha ili kuzuia Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani na kuishambulia kwa maneno makali kamati ya ujasusi katika bunge.

Rais wa Marekani alisema kwa FBI ilitumia muda mwingi kuchunguza Urusi kabla ya kuilaumu kwa kupuuzia alama za onyo ya mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 17 katika shule ya sekondari ya Florida Jumatano ya wiki iliyopita.

"Nasikitishwa sana kuona FBI kwa kutojali ishara zote zilizotumwa na mshambuliaji wa shule ya sekondari huko Florida. Haikubaliki," aliandika Donald Trump kwenye akaunti yake ya Twitter.