MAREKANI-ISRAEL-UBALOZI-JERUSALEM

Marekani kuhamishia Ubalozi wake mjini Jerusalem mwezi Mei

Mji wa Jerusalem, unaowaniwa kati ya Israel na Palestina
Mji wa Jerusalem, unaowaniwa kati ya Israel na Palestina REUTERS/Ronen Zvulun.

Marekani imesema itahamisha rasmi Ubalozi wake nchini Israel kutoka mjini Telviv kwenda Jerusalem mwezi Mei mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje, imethibitisha hili na kuhamishwa huko kutafanyika wakati Israel ikisherehekea miaka 70 ya uhuru wake.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, amekasirishwa na tangazo hili na kusema uamuzi huu wa Marekani haukubaliki.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepongeza hatua hiyo ya Marekani na kumshukuru rais Donald Trump, kwa uongozi mahiri na urafiki wa dhati kati ya mataifa hayo mawili.

Uamuzi huu wa Marekani unatarajiwa kusababisha kuendelea kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina na kurudisha nyuma juhudi za mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili.