MAREKANI-USALAMA

Mwalimu akamatwa akiwa na bunduki darasani Marekani

Hali ya usalama yadhibitiwa katika katika shule ya sekondari ya Dalton High School, kilomita 145 kaskazini mwa Atlanta.
Hali ya usalama yadhibitiwa katika katika shule ya sekondari ya Dalton High School, kilomita 145 kaskazini mwa Atlanta. REUTERS/Sait Serkan Gurbuz

Mwalimu mmoja aliyejihami kwa bunduki ndogo aina ya bastola ameripotiwa kufyatua risasi baada ya kujificha darasani katika shule ya sekondari ya Dalton High School, mjini Georgia nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mwalimu huyo alifyatua risasi wakati mkuu wa shule hiyo alikua akijaribu kufungua mlango. Lakini hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, polisi imesema baada ya kumkamata mwalimu huyo.

Tukio hili lililofanyika katika shule ya sekondari ya Dalton High School, kilomita 145 kaskazini mwa Atlanta, linatokea siku ambayo visomo vinaanza tena katika shule ya Marjory Stoneman Douglas High School mjini Parkland katika jimbo la Florida, ambapo watu 17 waliuawa na kijana mwenye umri wa miaka 19 siku 15 zilizopita.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wanafunzi ambao walitaka kuingia chuoni waligundua kwamba mwalimu wao hakuwakubalia waingie.

Mkuu wa shule alipofika na kujaribu kufungua mlango kwa ufunguo, risasi zilisikika ndani ya darasa hilo, hali ambayo ilipelekea ploisi kkuzindua utaratibu wa usalama na kuondoa wanafunzia katika shule hilo, lenye wanafunzi 2,000.

Polisi ya Dalton waligundua kuwa mwalimu huyo, aliyekua akitoa visomo vya sayansi ya jamii, alijificha darani akiwa amejihami kwa bunduki. Alikamatwa laiki sababu ya hatua yake haijaelezwa.

Profesa Jesse Randal Davidson, mwenye umri wa miaka 53, ameshtakiwa kwa kosa la kujaribu kufanya mashambulizi, kubebelea silaha ndani ya shule, vitisho vya kigaidi na utovu hatari wa nidhamu.

Mkuu wa shule, Steve Bartoo, alisem akatika mkutano na waandishi wa habari kwamba Jesse Randal Davidson alikuwa mwalimu mzuri, anayetegemewa sana katika shule hiyo.