Pata taarifa kuu
MAREKANI-SWEDEN-KOREA KASKAZINI

Marekani na Korea Kaskazini katika mazungumzo ya kuwaachia wafungwa 3

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un na rais wa Marekani Donald Trump.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un na rais wa Marekani Donald Trump. DR
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
2 Dakika

Nchi ya Korea Kaskazini iko kwenye mazungumzo na nchi za Marekani na Sweden kuangalia uwezekano wa kuwaachia huru wafungwa watatu wa Marekano, wakati huu shughuli za kidiplomasia zikishika kasi kabla ya kufanyika kwa mkutano kati ya utawala wa Pyongyang, Washington na Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Mzungumzo ya kuachiwa kwa raia hao wa Marekani wenye asili ya Korea yanaendelea kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni zaidi ya juma moja tangu rais Donald Trump akubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Utawala wa Pyongyang hata hivyo mpaka sasa haujathibitisha mkutano wake na rais Trump, mchakato ulioanzishwa na mjumbe wa Korea Kusini ambaye majuma kadhaa yaliyopita alionana na Kim Jong-Un.

Uamuzi wa rais Trumo kukubali mkutano na Jong-Un umeasha mchakato mpya wa taifa hilo kusaka ajenda ya mazungumzo kati ya viongozi hao wawili.

Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa juma imesema kuwa nchi ya Marekani na Korea Kaskazini zimefikia makubaliano ya awali katika kuachiliwa huru kwa wafungwa hao watatu Kim Hak-song, Kim Sang-duk na Kim Dong-chul.

Mwanadiplomasia wa Korea Kusini amenukuliwa akithibitisha kuwepo kwa mazungumzo hayo na kwamba hivi sasa makubaliano ya mwisho yanafanyika kuwezesha kuachiwa kwa wafungwa hao.

Mazungumzo ya kuachiwa kwa wafungwa haya yameelezwa kuratibiwa na umoja wa Mataifa na wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani.

Kuachiwa kwa wafungwa hawa kunaelezwa pia kulikuwa ni ajenda ya mazungumzo ya mjini Stockholm kati ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho na mwenzake wa Sweden Margot Wallstrom.

Nchi ya Sweden imeripotiwa kuwa muwakilishi wa matakwa ya Marekani kwa Korea Kaskazini.

Kim Dong-chul mchungaji raia wa Marekani na Korea Kusini alikamatwa tangu mwaka 2015 kwa tuhuma za kufanya ujasusi na baadae kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 na kazi ngumu mwaka 2016.

Kim Hak-song na Kim Sang-duk wote walikuwa wakifanya kazi katika chuo kikuu cha  Sayansi cha Pyongyang walikamatwa mwaka uliopita kwa tuhuma za kufanya shughuli zilizohatarisha usalama wa taifa.

Wadadisi wa mambo wanasema kuwa mazungumzo haya ya kuachiwa kwa wafungwa huenda kukarahisisha zaidi mazungumzo yaliyopangwa kufanyika kati ya Marekani na Serikali ya Pyongyang.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.