FACEBOOK

Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg aomba radhi kwa watumiaji wake

Nembo ya mtandao wa kijamii wa Facebook, ambayo sasa iko kwenye kashfa kubwa ya kuruhusu taarifa za wateja wake kudukuliwa.
Nembo ya mtandao wa kijamii wa Facebook, ambayo sasa iko kwenye kashfa kubwa ya kuruhusu taarifa za wateja wake kudukuliwa. REUTERS/Yves Herman/Foto Archivo

Mkurugenzi mkuu na mmliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amevunja ukimya juma hili kuhusu kashfa iliyoikumba kampuni yake ambapo ameomba radhi kutokana na "kuvunja uaminifu" na weteja wake zaidi ya bilioni moja na kuapa kutorudia makosa yaliyojitokeza.

Matangazo ya kibiashara

Katika matamshi yake ya kwanza kwa uma kuhusiana na matumizi mabaya ya taarifa binafsi za wateja zaidi ya milioni 50 kulikofanywa na kampuni ya Uingereza iliyokuwa na uhusiano na timu ya kampeni ya rais Donald Trump mwaka 2016, Zuckerberg amewaambia watumiaji wa Facebook kuwa taasisi yake "ilikuwa na wajibu wa kulinda taarifa zai."

Zucke ameongeza kuwa kama isingetokea, "basi hatuwastahili."

Ameahidi pia kuwa Facebook itachunguza kila programu iliyopata mwanaya wa kupitia akaunti za wateja wake na kufanya uchunguzi wa kisayansi kwa kitu chochote kilichoonekana kina wasiwasi.

"Hii ilikuwa ni uvunjifu mkubwa wa matumizi ya taarifa binafsi na uaminifu, nawaomba msamaha kwa kile kilichotokea," alisema Zuckerberg wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Marekani CNN.

Muanzilishi wa mtandao wa kijamii wa facebook, Mark Zuckerberg.
Muanzilishi wa mtandao wa kijamii wa facebook, Mark Zuckerberg. REUTERS/Stephen Lam/File Photo

"Wajibu wetu sasa ni kuhakikisha tukio hili halitokei tena."

Matamshi yake yamekuja baada ya siku kadhaa zambazo zimeshuhudiwa hisa za facebook zikianguka kwenye soko la dunia na kutolewa kwa wito wa uchunguzi ndani na nje ya nchi yake.

Imebainika kuwa kampuni ya Uingereza Cambridge Analytica ilifanikiwa kudukua taarifa binafsi za mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facbook kupitia progarmu maalumu ya utafiti uliofanywa na Aleksander Kogan na ambayo ilipakuliwa na mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo lakini kuchukua taarifa za marafiki wengine.

"Hiki kilikuwa kitendo cha uvunjifu wa uaminifu kati ya Kogan, Cambridge Analytica na Facebook," aliandika Zuckerberg. "Lakini ni kuvunja uaminifu kati ya Facebook na watu ambao wametoa taarifa zao kwetu na walitarajia tuzilinde."