Mahakama Kuu ya Brazil yamuhukumu Lula kifungo cha miaka 12
Imechapishwa:
Mahakama Kuu ya Brazil (STF) imemuhukumu rais wa zamani wa Brazili Luiz Inancio Lula da Silva kifungo cha miaka 12. Majaji 11 ndio walitakiwa kutoa uamuzi wao kuhusu hatima ya Lula da Silva.
Mapema siku ya Jumatano Luiz Inacio Lula da Silva, mwenye umri wa miaka 72, alisema ana matumaini kwamba mahakama ya juu zaidi nchini humo "itakubali hoja ya kutomuweka jela" mpaka kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.Mahakama ilifutilia mbali ombi hilo kwa kura sita dhidi ya tano.
Rais wa zamani wa Brazil Lula anaweza kutupwa jela siku zijazo.
Katika uchaguzi wa urais ujao wa mwezi Oktoba kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto alikua anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Katika Mahakama ya Rufaa, Luiz Inacio Lula da Silva alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na mwezi mmoja kwa kosa la rushwa.
Lula da Silva alipatikana na kosa la rushwa linalojulikana kama ''Operation Car Wash''
Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani ya euro laki saba na tisini.
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali, waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da silva aachiwe huru.
Baadhi ya watu wanapinga kuachiwa huru kwa Lula Da Silva na badala yake jeshi ndio liongoze nchi hiyo.