MAREKANI-TRUMP-SIASA

James Comey: Trump "hafai" kuongoza Marekani

Kitabu alichokiandika aliyekuwa Mkurugenzi wa  FBI James Comey.
Kitabu alichokiandika aliyekuwa Mkurugenzi wa FBI James Comey. REUTERS/Soren Larson

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumapili alimtusi kwa mara nyingine Mkurugenzi wa zamani wa shirika la ujasusi la nchi hiyo, FBI, James Comey, ambaye katika mahojiano yaliyorushwa jioni kwenye runinga ya ABC, alisema rais wa Marekani "hafai kuongoza Marekani".

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa zamani wa FBI, ambaye Trump alimfukuza mnamo mwezi Mei 2017, amerejelea habari za kisiasa za Marekani tangu kuchapishwa juma lililopita, maelezo mafupi ya kitabu chake kitakachotolewa siku ya Jumanne wiki hii.

Katika kitabu hicho "A Higher Loyalty, Truth, Lies and Leadership" amemfananisha rais wa Marekani na kiongozi wa kundi kutoka jamii ya mafia.

Katika mahojiano ya muda mrefu na ABC yaliyorushwa Jumapili usiku, Mkurugenzi wa zamani wa FBI anasema kwamba Trump "hafai kimaadili" kutekeleza majukumu yake ya urais na  amefanya "uharibifu mkubwa" kwa viwango vya taasisi za Marekani .

"Kimaadili hafai"

"Sijasema kuwa ana tatizo la akili kwa kuwa rais, ninasema hafai kimaadili kuwa rais," Bwana Comey amesema.