MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Donald Trump amwalika Vladimir Putin nchini Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amemwalika mwenzake wa Urusi Vladimir Putin nchini Marekani wakati wa mazungumzo ya simu kati ya wawili hao, limearifu shirika la habari la RIA Novosti likinukuu wizara ya mambo ya nje ya Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump akikutana na mweznake wa Urusi Hambourg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump akikutana na mweznake wa Urusi Hambourg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Likinukuu maneno ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, shirika hilo limesema Donald Trump amelingumzia mara kwa mara suala la mwaliko huu wakati wa mkutano wake na Putin.

Rais wa Marekani pia amesema kuwa atakuwa na furaha ya kutembelea Urusi, kwa mujibu wa shirika la habari la RIA Novosti.

Kwa upande mwingine, Sergei Lavrov amesema kuwa Urusi haitapendekeza kuhudhuria mkutano kati ya Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Bw LAvrov amesema anaamini kwamba Trump na Putin hawataki makabiliano ya kijeshi kati ya nchi zao baada ya mashambulizi ya nchi za Magharibi nchini Syria.