CHILE-PAPA FRANCIS-KANISA KATOLIKI

Maaskofu 34 wa Chile wajiuzulu

Maaskofu wa Chile waendelea kukumbwa na shutma za unyanyasaji wa kingono.
Maaskofu wa Chile waendelea kukumbwa na shutma za unyanyasaji wa kingono. REUTERS

Maaskofu 34 wa Chile, wanaoitishwa wiki hii Vatican kwa mkutano wa kujadili mgogoro kuhusu kashfa za unyanyasaji wa kingono, wamewasilisha barua yao ya pamoja ya kujiuzulu kwa Papa Francis, kulingana na taarifa iliyotolewa Ijumaa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Haijulikani kama papa atakubali kujiuzulu kwa viongozi wa hao wa kanisa Katoliki nchini Chile, au baadhi yao.

Katika taarifa yao, maaskofu wanaomba msamaha kwa Chile, waathirika na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani.

Wakati wa ziara yake nchini Chile mnamo mwezi Januari mwaka huu, Papa Francis alimtetea Askofu Juan Barros, akwa kuficha visa vya unyanyasaji wa kijinsia katika Kanisa la Chile.

Uchunguzi ulifanyika papo hapo na Askofu mkuu Charles Scicluna.

Askofu Scicluna alifanya uchunguzi, kwa ombi la papa, kuhusu askofu Juan Barros, aliyeteuliwa na Papa Francis mwaka 2015 akiwa mkuu wa dayosisi ndogo ya Osorno, kusini mwa Santiago, wakati ambapo alishtumiwa kuficha uhalifu wa unyanyasaji wa kingono uliofanywa na mshauri wake, Fernando Karadima.

Kwa matokeo ya uchunguzi huu, Papa mwezi uliopita alikiri kuwa amefanya "makosa makubwa" kwa jinsi alivyoshughulikia kesi hii kwa sababu alikosa "taarifa za kuaminika na zenye usawa".

Fernando Karadima, mwenye umri wa miaka 87, kwa sasa anaishi katika nyumba ya watu waliostaafu nchini Chile. PMpaka sasa bado anakanusha shutma dhidi yake.