MAREKANI=URUSI-FBI-SIASA-USALAMA

Trump ataka uchunguzi kuhusu kuingiliwa katika kampeni zake za uchaguzi

Donald Trump aomba uchunguzi juu ya "kuingiliwa katika kampeni zake. Analishuku Shirika la ujasusi la FBI.
Donald Trump aomba uchunguzi juu ya "kuingiliwa katika kampeni zake. Analishuku Shirika la ujasusi la FBI. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Idara ya Sheria ichunguze iwapo kampeni zake ziliingiliwa na watu kutoka nje ya kamati iliyoongozwa na Robert Mueller iliyoundwa kumpigia kampeni.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anahitaji uchunguzi kufanyika ilikubaini kama shirika la upelelezi la FBI lilijipenyeza kuchunguza kampeni zake kwa maslahi ya kisiasa.

Akinukuliwa na vyombo vya habari huko Marekani, meya wa jiji la New York amesikika akisema shirika la upelelezi la FBI linatakiwa kutoa maelezo kuhusu taarifa zinazoenea kwamba walikuwa na watu wao wa siri kwenye mikutano ya ndani ya Trump kwa lengo la kumchunguza.

Hata hivyo Gazeti la New York Times lilichapisha taarifa iliyodai kuwa FBI walituma mtu wao kufuatilia mwenendo wa kampeni za Trump mara tu walipopata taarifa za uwezekano wa Urusi kuingilia uchaguzi huo.

Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter alikuwa na mfululizo wa madai ya kukanusha na kudai hakuna ushahidi wowote wa kuzihusisha kampeni zake na Urusi.