MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Mike Pence: Kim Jong-un nakuomba usithubutu kumchezea Trump

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence. REUTERS/Irakli Gedenidze

Wakati zikisalia siku chache kabla ya mkutano kati ya rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Juni 12, Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amemuonya kiongozi wa Korea Kaskazini kuwa asimchezee Rais Donald Trump ikiwa watakutana mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na Fox News Bw Pence amesema kuwa yatakua makosa makubwa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kufikiri kuwa atamchezea Donald Trump. Rais Donald Trump hana mchezo, ikiwa Kim Jong-un atamchezea Donald Trump hatosita kuondoka kwenye mkutano huo wa Juni 12.

“Hakuna shaka kuwa Donald Trump ana nia ya kuondoka kwenye mkutano huo ambao unapangwa kufanyiwa nchini Singapore, “ amesema Bw Pence.

Hayo yanajiri wakati ambapo hivi karibuni Korea Kaskazini ilitishia kujitoa katika mkutano huo baada ya mshauri wa masuala ya ya ulinzi nchini Marekani John Bolton kusema kuwa itafuata mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia za Korea Kaskazini.