MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Donald Trump: Kuna uwezekano mkutano na Kim Jong-un kuahirishwa

Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne, Mei 22, 2018 katika White House wakati akimpokea Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne, Mei 22, 2018 katika White House wakati akimpokea Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in. REUTERS/Kevin Lamarque

Mkutano wa kihistoria uliopangwa kufanyika Juni 12 nchini Singapore kati ya rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini bado haijulikani kama utafanyika.

Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amesisitiza kuwa hata hivyo Korea kaskazini itapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea.

Donald Trump, ambaye siku ya Jumanne wiki hii, alimpokea Rais wa Korea Kusini katika White House, alisema kuna uwezekano wa kusitishwa kwa mkutano huo.

Wiki tatu tu kabla ya mkutano huo ambao rais wa Marekani amekua akiendelea kusema kuwa ni wa kihistoria, bado kuna shaka juu ya kufanyika kwa mkutano huo wa kilele wa Singapore.

"Tumeweka baadhi ya masharti na nadhani tutapata kuridhika na vinginevyo mkutano hautafanyika, na katika hali hii, unaweza kufanyika baadaye. Mkutano huo unaweza kufanyika tarehe nyingine. Tutaona, "Donald Trump alisema.

Rais wa Marekani ameomba serikali ya Korea Kaskazini kuwajibika katika kuweka salama nchi yao. Kwa upande mwingine, Donald Trump ameahidi kuhakikisha usalama wa Kim Jong-un na kumhakikishia matarajio mazuri:

"Tutamhakikishia usalama wake na tuliongelea suala hilo tangu mwanzoni. Atakuwa salama, atakuwa na furaha, nchi yake itakuwa tajiri na katika kipindi cha miaka 25 au 50 ataangalia nyuma na kujivunia sana kwa kile alichokamilisha kwa Korea Kaskazini na ulimwengu wote. "