MAREKANI-WAHAMIAJI-HAKI

Mahakama yaagiza kuungana kwa familia zilizotenganishwa Marekani

Msichana mdogo kutoka El Salvador na mama yake aliyefungwa waungana kwenye kituo cha msaada cha Kanisa Katoliki huko McAllen, Texas, Juni 17, 2018
Msichana mdogo kutoka El Salvador na mama yake aliyefungwa waungana kwenye kituo cha msaada cha Kanisa Katoliki huko McAllen, Texas, Juni 17, 2018 © AFP

Mahakama ya San Diego (kusini-magharibi mwa Marekani) imeamuru kuungana kwa familia za wahamiaji zilizotenganishwa na Idara ya uhamiaji, huku ikishtumu sera ya serikali ya "kutovumilia".

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rais Donald Trump amepata ushindi mkubwa Jumanne wiki hii baada ya miezi kadhaa ya mvutano kuhusu marufu ya kusafiri kwa raia kutoka nchi sita zenye Waislam wengi.

Mahakama ya Juu nchini huo imeidhinisha marufuku hiyo tata inayolenga raia kutoka mataifa ya Iran, Libya, Somalia, Syria na Yemen.

Lakini sera yake ya "kutovumia" dhidi ya uhamiaji haramu, ambapo karibu majimbo 20 ya Marekani, ambayo hata hivyo yalifungua mashitaka, yanakabiliwa na shinikizo kwa siku kadhaa.

Kulingana na uamuzi wa Mahakama ya San Diego, wazazi wanapaswa kuungana (kukutana) na watoto wao kwa muda wa siku zisizozidi 14 kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5, na kwa muda wa siku zisizozidi thelathini kwa watoto wanaosalia, isipokuwa ikiwa watakua ni hatari kwa watoto hao. Uamuzi huo unaomba serikali ya Marekani "kukabiliana na mazingira tatanishi iliyosababisha".

Malalamiko yaliwasilishwa na shirika la Haki za binadamu la ACLU kwa niaba ya wahamiaji wasiojulikana dhidi ya Idara ya Uhamiaji (ICE), ambapo Jaji Dana Sabraw pia ameomba "kufanya kinachowezekana ili kuwezesha mawasiliano" kati ya familia zilizotenganishwa na kuwaruhusu kuzungumza kwa muda wa siku kumi.