MEXICO-MAREKANi-USHIRIKIANO

Rais mpya wa Mexico azungumza na Trump kuhusu suala la wahamiaji

Rais mpya wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador.
Rais mpya wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador. REUTERS / Alexandre Meneghini

Rais mpya wa Mexico Lopez Obrador amesema amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump, kuhusu changamoto za wahamiaji kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Obrador amesema, amezungumza na rais Trump kwa muda wa nusu saa kwa njia ya simu na pamoja na mambo ya uhamiaji, viongozi hao wamejadiliana kuhusu namna ya kuimarisha usalama na kuunda nafasi za kazi.

Rais Trump amesema anatumaini kuwa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaimarika baada ya Mexico kumpata rais mpya.

Andres Manuel Lopez Obrador kutoka mrengo wa kushoto, alishinda Uchaguzi wa urais dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ricardo Anaya.

Uchaguzi huu ulifanyika wakati ambapo raia wa nchi hiyo wamekua wakilalamikia kuhusu ongezeko la ufisadi na machafuko.