NATO-ULINZI-USALAMA

Mkutano wa NATO: Trump ahitilafiana na viongozi wengine kuhusu ongezeko la bajeti ya ulinzi

Mkutano wa NATO huko Brussels: Rais wa Marekani Donald Trump alitoa shinikizo washirika wake kwa kujaribu kuwahimiza kuwa na ongezeko katika bajeti yao ya ulinzi, Jumatano, Julai 11.
Mkutano wa NATO huko Brussels: Rais wa Marekani Donald Trump alitoa shinikizo washirika wake kwa kujaribu kuwahimiza kuwa na ongezeko katika bajeti yao ya ulinzi, Jumatano, Julai 11. U.S. President Donald Trump checks time prior to a dinner at the

Rais wa Marekani amewataka viongozi wengine wa nchi wanachama wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO kuongeza bajeti ya ulinzi, hali ambayo imezua mvutano kati ya mataifa wanachama wa umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais Donald Trump ameishtumu Ujerumani kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake.

Mkutano wa Brussels unakuja ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya Rais Trump kuwa na mkutano wa kwanza na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini mjini Helsinki nchini Finland.

Licha ya rais Trump kuhimiza washirika hao wa NATO kuwa na ongezeko la bajeti ya ulinzi,lakini wanachama wa NATO wamesema hayawezi kutimiza ahadi zao ifikapo mwaka 2024.

Rais Donald Trump amewataka washirika wa NATO kuongeza kiasi cha fedha mara mbili zaidi kwa ajili ya kuongeza bajeti ya ulinzi ambayo kwa sasa wanachangia asilimia mbili tu,na yeye akiwataka kufikia mchango wa asilimia nne kutoka kwenye pato la mataifa hayo.