MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Mkutano wa kihistoria kati ya Trump na Putin kufanyika Helsinki

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mwezi Julai 2017 huko Hamburg kando na mkutano wa G20.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mwezi Julai 2017 huko Hamburg kando na mkutano wa G20. REUTERS/Carlos Barria//File Photo

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano muhimu jijini Helnsiki nchini Finland. rump amesema anakwenda katika mazungumzo haya akiwa na matarajio madogo lakini anaamini kuwa, huenda kitu kizuri kitaafikiwa katika mkutano huo.

Matangazo ya kibiashara

Ni mkutano utakaofanyika, wakati huu raia 12 wa Urusi wakifunguliwa mashtaka nchini Marekani, kwa madai ya kuingilia Uchaguzi Mkuu mwaka 2016.

Hakuna ajenda maalum katika mkutano kati ya viongozi hawa wawili, ikiwa na maana kuwa, mambo mbalimbali yatajadiliwa.

Huu ni mkutano wa kwanza wa nchi hizi mbili katika kiwango hiki kati ya Rais wa Urusi na wa Marekani. Mkutano kama huu ulikua haujafanyika kwa miaka nane. Baada ya miezi kadhaa ya uhasama wa kidiplomasia, vikwazo, kufukuzwa kwa wanadiplomasia kwa misingi ya kesi ya Skripal, tuhuma za Urusi kuingilia katika mchakato wa uchaguzi wa Marekani, wala hakuna kinachotarajiwa kikubwa katika mazungumzo haya.

Huu ni mkutano ambao Donald Trump ametamani kwa muda mrefu, ambapo alihisi kuwa unaweza kuwa rahisi zaidi ikilinganishwa na ziara zake zote alizofanya barani Ulaya, kabla ya kusema katika mkutano na waandishi wa habari, "Putin si adui yangu,".