MAREKANI-NATO-USALAMA

Trump: Mkutano wa kilele wa NATO ulikuwa mzuri sana

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Marekani Donald Trump kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa NATO huko Brussels Julai 11, 2018.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Marekani Donald Trump kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa NATO huko Brussels Julai 11, 2018. REUTERS/Reinhard Krause

Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO akisema mkutano aliohudhuria jumalililopita, ulikua "wenye mafanikio.

Matangazo ya kibiashara

Bw Trump ameandika Jumatatu wiki hii kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi (NATO) ulikuwa "wenye mzuri sana", kinyume na kile "kilichozungumzwa na vyombo vingia vya habari" .

Rais wa Marekani, ambaye amehakikishia Umoja wa Ulaya uungaji wake mkono baada ya kuwaonya kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi yao ya kijeshi, amesema kuwa Muungano wa Atlantic umeonekana "wenye nguvu na tajiri" katika mkutano hu.

"Nilipokea simu nyingi kutoka kwa viongozi wa NATO ambao walinishukuru kwa kuwaunganisha na kuwafanya waweze kuzingatia majukumu yao ya kifedha," amesemasaa chache kabla ya mkutano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Katika mkutano wa NATO, rais Trump ahitilafiana na viongozi wengine kuhusu ongezeko la bajeti ya ulinzi, kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, vikinukuu vyanzo kutoka mkutano huo.

Rais wa Marekani amewataka viongozi wengine wa nchi wanachama wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO kuongeza bajeti ya ulinzi, hali ambayo imezua mvutano kati ya mataifa wanachama wa umoja huo.

Licha ya rais Trump kuhimiza washirika hao wa NATO kuwa na ongezeko la bajeti ya ulinzi,lakini wanachama wa NATO walisema hayawezi kutimiza ahadi zao ifikapo mwaka 2024.

Rais Donald Trump amliwataka washirika wa NATO kuongeza kiasi cha fedha mara mbili zaidi kwa ajili ya kuongeza bajeti ya ulinzi ambayo kwa sasa wanachangia asilimia mbili tu, na yeye akiwataka kufikia mchango wa asilimia nne kutoka kwenye pato la mataifa hayo.