CANADA-USALAMA

Tisa wajeruhiwa kwa kupigwa risasi Toronto

Watu kadhaa wajeruhiwa baada ya kupigwa risasi na mshambuliaji huko Toronto, Canada.
Watu kadhaa wajeruhiwa baada ya kupigwa risasi na mshambuliaji huko Toronto, Canada. Lars Hagberg / AFP

Watu wasiopungua tisa wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi Jumapili usiku mjini Toronto, nchini Canada, kwa mujibu wa polisi ya nchi hiyo. Mshambuliaji ameuawa, polisi imesema kwenye akaunti yake ya Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu w vituo vya habari vya CTV na CBS, watu waliojeruhiwa, ikiwa ni pamoja na msichana mdogo, walpelekwa hospitali baada ya kupigwa risasi, tukio lililotokea katika eneo la mashariki mwa jiji.

Waziri wa Ontario Doug Ford aandika kwenye ukurasa wake wa Twitter "Ninasikitishwa na tukio hilo baya kabisa lililotokea Toronto na tunawapa pole watu waliojeruhiwa pamoja na familia zao. Ninawashukuru watu wote walioshiriki haraka kwa kusaidia majeruhi."

Kwa upande wake, Meya wa mji wa Toronto, John Tory amewataka wakazi wa mji huo kujizuia kutoa habari za uzushi kuhusiana na tukio hilo. "Tunawaomba raia kujizuia kuzungumza chochote kuhusiana na tukio hili, kwa sababu Polisi ya Toronto haijamaliza uchunguzi wake. "