VENEZUELA-SISASA-SHAMBULIZI

Rais Maduro asema ameponea shambulizi la kumuua

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amesema amepotea chupuchupu jaribio la kumuua, baada ya kushambuliwa na ndege isiyolkuwa na rubani.

Rais Nicholas  Maduro wakati akiwahotubia wanajeshi wakati mlipuko uliposhuhudiwa Agosti 5 2018
Rais Nicholas Maduro wakati akiwahotubia wanajeshi wakati mlipuko uliposhuhudiwa Agosti 5 2018 DR
Matangazo ya kibiashara

Maduro amesema alilengwa wakati wa maadhimisho ya kijeshi jijini Carascas.

Picha zimemwonesha rais Maduro akiangalia angani ghafla, wakati alipokuwa anatoa hotuba yake.

Wanajeshi walionekana wakikimbia baada ya kushuhudiwa kwa mlipuko huo huku saba wakijeruhiwa na watu wengine wakikamatwa.

Maafisa wanasema kulitokea na mlipuko karibu na jukwaa alilokuwa ameketi rais Maduro.

“Lilikuwa shambulizi kutaka kuniua, walijaribu kuniua leo,” amesema rais Maduro akielezea namna alivyoshuhudia mlipuko mbele yake.

Rais Maduro ameishtumu Colombia kupanga kumuua, tuhma ambazo serikali ya nchi hiyo imekanusha vikali.

“Sina shaka kuwa, rais wa Colombia Juan Manuel Santos alikuwa nyuma ya shambulizi hili,” amesema.