COLOMBIA-SIASA-USALAMA

Iván Duque: Ninapanga kuliunganisha taifa letu lililogawanyika

Ivan Duque ametawazwa kuwa rais wa Colombia kwa muhula wa miaka minne,Jumanne Agosti 7, 2018 huko Bogota.
Ivan Duque ametawazwa kuwa rais wa Colombia kwa muhula wa miaka minne,Jumanne Agosti 7, 2018 huko Bogota. Fabian Ortiz/Courtesy of Colombian Presidency/Handout via REUTER

Rais mpya wa Colombia Iván Duque, ambaye anatajwa kuwa mdogo zaidi kuwahi kutawala taifa hilo, amepiashwa na kuanza kuongoza taifa hilo la Amerika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo mpya anamrithi rais aliyemaliza muda wake Juan Manuel Santos, baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu mwezi Juni.

Akiwahotubia raia wa Colombia kwa mara ya kwanza akiwa rais , Duque ameahidi kuliunganisha taifa hilo na kuimarisha hali ya uchumi.

Aidha, Wakili huyo wa zamani ameahidi kupambana na ufisadi na wale wanaofanya makosa ya kuhujumu uchumi.

Pamoja na hayo yote, kiongozi mpya amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa ana nia ya kuufanyia marekebisho mkataba wa amani uliofikiwa kati ya serikali iliyopita na waasi wa FARC.

Tangu mkataba huo mwaka 2016, FARC kimekuwa chama cha kisiasa na kinawakilishwa bungeni.

Rais wa zamni Santos amemtaka rais huyu mpya kuheshimu mkataba huo wa amani.