MAREKANI-URUSI-VIKWAZO

Marekani yatishia kuiwekea vikwazo vipya vya kiuchumi Urusi

Maafisa wa OPCW huko Salisbury katika eneo la shambulio kwa sumu dhidi aliyekuwa jasusi wa nchi yake na Uingereza Sergei Skripal na binti yake Yulia
Maafisa wa OPCW huko Salisbury katika eneo la shambulio kwa sumu dhidi aliyekuwa jasusi wa nchi yake na Uingereza Sergei Skripal na binti yake Yulia REUTERS/Peter Nicholls

Marekani imetangaza kuwa itaiwekea Urusi vikwazo vipya baada ya kubaini kuwa ilitumia sumu kumshambulia aliyekuwa jasusi wa nchi yake na Uingereza Sergei Skripal na binti yake Yulia mwezi Machi.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka katika Wizara ya Mambo ya nje imesema, inatekeleza hatua dhidi ya Urusi, ambayo kiongozi wake Vladimir Putin amekanusha kuhusika.

Hata hivyo, uchunguzi wa Uingereza umeibaini kuwa, shambulizi hilo lilitekelezwa na serikali ya Urusi.

Marekani imesema vikwazo hivyo, vitaanza kutekelezwa kuanzia tarhehe 22 mwezi huu na ni pamoja na kuizuia kuingiza bidhaa vya kieletroniki na vingine vinavyohusu teknolojia.

Aidha, Washington DC imeonya kuwa, vikwazo zaidi vitafuata baada ya siku tisini iwapo Urusi haitasema kuwa, haitatumia tena silaga za kemikali.

Marekani pia inaitaka Urusi kukubali Umoja wa Mataufa kwenda kuchunguza hifadhi zake za silaha za kemikali.

Uingereza imepongeza hatua hii ya Marekani.