HONDURAS-MAZUNGUMZO-SIASA

Wadau washindwa katika jaribio jipya la mazungumzo Honduras

Upinzani nchini Hondurans unaomba rais Hernandez kujiuzulu.
Upinzani nchini Hondurans unaomba rais Hernandez kujiuzulu. Fuente: Reuters.

Mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kati ya upinzani na serikali ya Honduras ili kuondokana na mgogoro wa kisiasa uliofuata uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba yalishindwa kuanza tena Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

"Kile kilichotokea kinasikitisha sana kwa wananchi wa Honduras ambao hawakuta iwe hivyo," alisema mwakilishi wa Umoja wa Mataifa hulo Tegucigalpa, Igor Garafulic, baada ya mkutano uliolenga kutafuta makubaliano ya kuanza tena kwa mazungumzo ambayo yalifeli mapema mwezi Julai.

Wawakilishi wa rais Juan Orlando Hernández, kutoka chama cha National Party (mrengo wa kulia), Liberal Party (mrengo wa kulia) na kiongozi wa upinzani Salvador Nasralla, mtangazaji kwenye televisheni na mgombea wa zamani wa muungano wa upinzani dhidi ya utawala wa kiimla (mrengo wa kushoto) katika uchaguzi wa mwisho wa urais, wamekua wakihudhuria mkutano huo.

"Umoja wa Mataifa umeweka wapatanishi na wawezeshaji ambao wako tayari kuendeleza mazungumzo hayo lakini wakati huu, hali ya kutoaminiana kati ya wanasiasa wa Honduras inaonesha kuwa ni vigumu kuendelea kwa mazungumzo hayo," amesema Bw Garafulic.

Tony Garcia, kwa niaba ya Nasralla, amebaini kwamba mazungumzo hayo yalikuwa yamesimama kwa ombi la chama cha National Party la kuwa na mwakilishi sambamba na mjumbe wa rais, "jambo ambalo hatuwezi kukubali."

"Kushindwa kwa mazungumzo haya kumesababishwa na chama cha National Party," amesema Enrique Ortez wa Liberal Party.

Polisi ikijaribu kutawanya maandamano ya upinzani huko Tegucigalpa, Honduras.
Polisi ikijaribu kutawanya maandamano ya upinzani huko Tegucigalpa, Honduras. REUTERS/Edgard Garrido