MAREKANI-TRUMP-HAKI

Donald Trump ajikuta matatani baada ya kushtumiwa na mwanasheria wake wa zamani

Mwanasheria wa zamani wa Donald Trump, Michael Cohen akitoka mahakamani huko New York Agosti 21, 2018.
Mwanasheria wa zamani wa Donald Trump, Michael Cohen akitoka mahakamani huko New York Agosti 21, 2018. REUTERS/Mike Segar

Rais wa Marekani Donald Trump amepata pigo kubwa mara mbili katika kesi mbili ambazo ameonekana kuhusika. Jumanne wiki hii, Paulo Manafort, meneja wake wa zamani wa kampeni, alipatikana na hatia ya udanganyifu wa kodi na masuala ya kibenki kwa mashtaka nane kati ya 18 yanayomkabili.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Michael Cohen, wakili wa zamani wa Donald Trump, alikiri mashtaka nane, sita ya udanganyifu wa kodi na benki na mashitaka mawili yanayohusiana na kufadhili kampeni ya uchaguzi kinyume cha sheria. Mbaya zaidi, mwanasheria wa zamani wa rais alihakikishia mahakamani kuwa alikiuka sheria kwa ombi la rais.

Hili ni pigo kubwa kwa rais wa Marekani baad ay kuhusihwa na mtu ambaye alikua akimuamini kwa zaidi ya muongo mmoja. Michael Cohen alieleza mwenyewe kuwa ni mtu wa karibu wa Donald Trump. Alisema kuwa alikuwa akihusika na kutatua matatizo yake. Lakini mwanasheria huyo wa zamani wa rais Trump sasa anaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa kwa Donald Trump.

Mbele ya Mahakama, Michael Cohen alidai alilipa dola 130,000 na 150,000 kwa wanawake wawili ili kuwaziba midomo kuhusu mahusiano yao na Donald Trump kwa ombi la Donald Trump kwa lengo la kushawishi uchaguzi.

Taarifa ambayo ina maana kuwa rais alifanya kosa. Michael Avenatti, mwanasheria wa Stany Daniels, mmoja wa wanawake hawa wawili, amesisitiza kuhusika wa Donald Trump juu ya suala hili. "Rais alisema akiwa katika ndege ya Air Force One kwamba hajui kuhusu muamala wa malipo ya dola 130,000, lakini sasa tunajua ukweli kutoka kwa Michael Cohen, na tunaweza kusema kuwa rais wa Marekani alidanganya wananchi wa Marekani. wakati alikuwa ndani ya ndege ya wananchi wa Marekani. "

Michael Cohen amekata rufaa katika mahakama ya Manhattan dhidi ya madai yanayomkabili kwamba alikiuka sheria za uchaguzi, na kudai kuwa alifanya hivyo kwa uongozi wa "mgombea", kwa lengo la kupitisha uchaguzi salama.

Michael Cohen alikuwa chini ya uchunguzi maalum kutokana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kuweko uwezekano wa udanganyifu dhidi yake juu ya masuala ya benki na ushuru.