Wanne wauawa katika eneo la burudani Florida
Imechapishwa:
Watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine kumi wamejeruhiwa wakati wa mashindano ya mchezo wa video katika eneo la burudani la Jacksonville, katika Jimbo la Florida, nchini Maekani, polisi na vyombo vya habari wamebaini. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili.
Mshambuliaji, ambaye ni mzungu, ni miongoni mwa watu waliouawa, amesema Mike Williams, mkuu wa mji huo.
Mji wa Jacksonville unapatikana kilomita sitini kusini mwa mpaka na Georgia kwenye pwani ya Atlantiki.
Magari kadhaaya wagonjwa yalitumwa eneo la tukio, tukio ambalo lilitokea katika mgahawa wa pizza Jacksonville Landing, huko Chicago, eneo la burudani na biashara, ambapo kulikua kukifanyika mashindano ya Madden 19, mchezo wa soka wa Marekani.
Tukio hili lilirushwa kupitia mitandao ya kijami, huku wachezaji wakionekana wakikabilianna na mshambuliaji, lakini kelele zimekua zikisikika.
Kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times, mshambuliaji ni mmoja wa wachezaji ambaye alifyatua risasi baada ya kushindwa. Kisha alijiua, limeongeza gazeti hilo, ambalo limenukuu ujumbe wa mchezaji mwingine.
Mnamo mwezi Februari, watu 17 waliuawa katika mkasa kama huo katika shule ya Parkland, katika Jimbo la Florida, na watu wengine 49 waliuawa katika mazingira kama hayo, miaka miwili iliyopita huko Orlando.