MAREKANI

Marais wa zamani wa Marekani waongoza heshima za mwisho kwa Seneta McCain

Marais wa zamani wa Marekani wakiwa mstari wa mbele katika maziko ya Seneta John McCain katika Kanisa la Washington Septemba 1,2018
Marais wa zamani wa Marekani wakiwa mstari wa mbele katika maziko ya Seneta John McCain katika Kanisa la Washington Septemba 1,2018 REUTERS/Chris Wattie

Marais wawili wa zamani kutoka vyama pinzani nchini Marekani wameungana kumpa heshima za mwisho seneta wa zamani John McCain katika ibada ya maziko iliyotilia mkazo matarajio yake ya umoja wa kisiasa na kukemea ukabila na mgawanyiko unaowekwa na rais wa sasa Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Wakati mamilioni walkifuatilia maziko hayo ya kihistoria yaliyohudhuriwa na marais wa zamani Barack Obama na George W Bush kupitia televisheni ya taifa, rais Trump hakuwepo na badala yake alielekea kwenye klabu yake ya golf huko Virginia.

Naye Binti wa seneta McCain, Meghan alipata nafasi ya kuzungumza baada ya marais hao wa zamani ambapo alitumia maneno ya rais Trump wakati wa kampeni kwa namna nyingine akisema Marekani ya McCain haihitaji kufanywa kubwa tena kwa kuwa Marekani ni kubwa siku zote.