BRAZIL-LULA-HAKI

Lula kuwasilisha maombi yake mbele ya Umoja wa Mataifa na Mahakama Kuu

Wafuasi wa Lula wakiandamana wakidai kiongozi wao aachiliwe huru huko Brasilia, Agosti 14, 2018.
Wafuasi wa Lula wakiandamana wakidai kiongozi wao aachiliwe huru huko Brasilia, Agosti 14, 2018. REUTERS/Adriano Machado

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anatarajia kuwasilisha maombi yake mawili mbele ya Umoja wa Mataifa na Mahakama Kuu nchini Brazil ili kujaribu kuwania katika uchaguzi ujao baada ya kuzuiwa na mahakama ya uchaguzi, mgombea mwenza amesema.

Matangazo ya kibiashara

Wanasheria wa Lula wataomba taasisi hizo mbili kufuta utekelezaji wa hukumu ambayo Mahakama Kuu ya Uchaguzi (TSE) ilitoa siku ya Ijumaa na kubaini kwamba Lula, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 12 kwa kosa la rushwa na kujitajirisha kinyume cha sheria hana sifa ya kuwania katika uchaguzi wa urais.

Hivyo, "hakutakuwa na haja ya kuchukua nafasi ya (Lula) katika siku kumi zilizotolewa na TSE," amesema Fernando Haddad.

Meya wa zamani wa Sao Paulo, ambaye ni mgombea mwenza wa Lula katika uchaguzi wa tarehe 7 na 28 Oktoba, alikutana na rais wa zamani wa Brazil huko Curitiba, kusini mwa nchi, ambako anazuiliwa.

"Uamuzi wa chama ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa TSE na leo tumemuonyesha Rais Lula uwezekano wa kisheria mbele yake na alichukua uamuzi wake, kupitia wanasheria wake," amesema Fernando Haddad.

Fernando Haddad, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Lula katika kinyang'anyiro cha urais kwa niaba ya chama cha Labour.
Fernando Haddad, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Lula katika kinyang'anyiro cha urais kwa niaba ya chama cha Labour. REUTERS/Rodolfo Buhrer