MEXICO-USALAMA

Miili 166 yagunduliwa katika kaburi la halaiki Mexico

Jimbo la Veracruz ni mojawapo ya Majimbo yalioathiriwa na machafuko na uhalifu, ikiwa ni pamoja na makundi yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya.
Jimbo la Veracruz ni mojawapo ya Majimbo yalioathiriwa na machafuko na uhalifu, ikiwa ni pamoja na makundi yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya. REUTERS/Oscar Martinez

Polisi nchini Mexico imegundua miili mia moja na sitini na sita katika kaburi la halaiki katika Jimbo la Veracruz, mashariki mwa nchi hiyo, mwendesha mashitaka wa eneo hilo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Mapema mwezi Agostia, wachunguzi waligundua miili katika makaburi 32 katika eneo la katikati mwa jimbo hilo baaada ya kupata taarifa kutoka kwa mtu asiyejulikana, mwendesha mashitaka Jorge Winckler amesema katika mkutano na waandishi wa habari, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu eneo ambako kaburi hilo la halaiki limepatikana.

Jimbo la Veracruz ni mojawapo ya Majimbo yalioathiriwa na machafuko na uhalifu, ikiwa ni pamoja na makundi yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya.

Mnamo mwezi Machi 2017, mwendesha mashitaka Winckler alitangaza kwamba fuvu 250 ziligunduliwa katika makaburi yasiyojulikana katika Jimbo la Veracruz.