MAREKANI-CHINA-BIASHARA-USHURU

Marekani yaongeza ushuru kwa bidhaa kutoka China

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump 路透社

Marekani imetangaza ushuru mpya wa asilimia 10 kwa bidhaa kutoka nchini China zinazoingia nchini humo, suala ambalo linatarajiwa kuleta msuguano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.  

Matangazo ya kibiashara

Ushuru huu unalenga bidhaa zenye thamani ya Dola Bilioni 200, zinazoingizwa nchini Marekani.

Rais  Donald Trump, ametangaza kuwa ushuru huu utaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 24 mwezi huu wa Septemba.

Miongoni mwa bidhaa ambazo zimelengwa katika ushuru huo ni pamoja na pochi za wanawake, mchele na nguo.

Hata hivyo, saa na viti maalum za juu hazijawekwa katika orodha hiyo,

Hatua hii inalega kuendeleza vita vya kibiashara kati ya Marekani na China,baada ya Beijing kuonya kuwa haitakubali tena bidhaa zake kutozwa ushuru zaidi.

Iwapo mwafaka hautapatikana, Marekani itaongeza utozwaji huu kufikia aislimia 25 kuanzia mwaka ujao.