MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Jaji Kavanaugh aendelea kukabiliwa na mashitaka ya unyanyasaji wa kimapenzi

Brett Kavanaugh mbele ya Kamati ya sheria ya Bunge la Seneti, siku ya tatu akisikilizwa, Septemba 6, 2018, Washington.
Brett Kavanaugh mbele ya Kamati ya sheria ya Bunge la Seneti, siku ya tatu akisikilizwa, Septemba 6, 2018, Washington. REUTERS/Alex Wroblewski

Mwanamke wa pili amejitokeza na kudai kuwa alinyanyaswa kimapenzi na Brett Kavana aliyependekezwa na rais wa Marekani Donald Trump, kuwa Jaji katika Mahakama ya Juu.

Matangazo ya kibiashara

Deborah Ramirez, mwnye umri wa miaka 53, anatarajiwa kusikilizwa na Bunge la Seneti siku ya Alhamisi kuhusu madai haya ya unyanyasaji wa kijinsia ambao anadai kuwa alifanyiwa.

Wakati huo huo Maseneta kutoka chama cha Democratic wanaendelea kuchunguza madai hayo, baada ya mwanamke huyo Deborah Ramirez mwenye umri wa miaka 53, kudai kuwa alinyanyaswa na Kavanaugh wakati akiwa Chuo Kikuu cha Yale.

Shutuma hizi mpya dhidi mshirika wa karibu wa Donald Trump ni za tangu miaka ya 80.

Deborah Ramirez na Christine Blasey Ford wanatarajiwa kusikilizwa siku ya Alhamisi na Bunge la Senate kuhusu madai hayo.

Kavana amekuwa akikanusha madai dhdi yake akisema yanalenga kumchafulia jina na kumzuia kuchukua nafasi ya kuwa Jaji katika Mahakama hiyo.