MAREKANI-IRAN-USHIRKIANO

Marekani yaionya Iran kwa mara nyingine

Askari waliouawa na wengine kujeuhiwa kufuatia mashambulizi dhidi ya gwaride la wanajeshi huko Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, Septemba 22, 2018.
Askari waliouawa na wengine kujeuhiwa kufuatia mashambulizi dhidi ya gwaride la wanajeshi huko Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, Septemba 22, 2018. ALIREZA MOHAMMADI / ISNA / AFP

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Haley ameitaka nchi ya Iran kujitazama kwanza kwa kusababisha shambulio la mwishoni mwa juma ambalo lilisababisha vifo vya watu 25 wakiwemo raia wa kawaida na wanajeshi.

Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Haley yamekuja siku chache tu baada ya utawala wa Tehran kuituhumu Marekani na washirika wake kufadhili makundi ya kigaidi yaliyotekeleza shambulio la mwishoni mwa juma.

Akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Marekani cha ABS Haley amesema akisisitiza kutohusika kwa nchi yake na kuitaka Iran kuacha kutafuta mchawi.

Nchi hizo mbili kwa miongo kadhaa zimekuwa katika uhusiano mbaya ambapo Marekani imekuwa ikiilaumu Iran kwa kwa kuzalisha silaha za kinyuklia jambo ambalo Iran imekuwa ikilakanusha ziku zote.

Matamshi ya Marekani yanakuja wakati siku ya Jumanne wakuu wa nchi kutoka mataifa mbalimbali duniani watahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa huku ajenda ya Iran na Korea Kaskazini zikitarajiwa kutawala mkutano huu wa mwaka.