UN-USHIRIKIANO

Viongozi mbalimbali wa dunia kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Kwenye upande wa kushoto, makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.
Kwenye upande wa kushoto, makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. (Photo : Wikimedia)

Mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja wa Mataifa unafunguliwa Jumanne wiki hii kwa hotuba za viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hotuba za marais wa Marekani Trump, Macron wa Ufaransa na Hassan Rouhani wa Iran.

Matangazo ya kibiashara

Marais na viongozi wa serikali zaidi ya 130 wanatarajia kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka huu. Umoja wa Mataifa unataka kuona kupitia takwimu hii ushahidi tosha kuwa ushirikiano wa kimataifa hauna matatizo, lakini utakuwa na kibarua kigumu cha kuwashawishi viongozi hao kuhusu ukosefu wa mafanikio katika migogoro mikubwa nchini Syria, Yemen, Libya au hata Burma.

Mkutano Mkuu unafunguliwa katika hali yake ya kipekee wakati bado nchi kadhaa zinaendelea kukabiliwa na machafuko, huku baadhi ya nchi zikiendelea kuwa na uhasama. Viongozi 130 wanatarajia kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikilinganishwa na 114 mwaka jana.

Lakini baadhi ya viongozi wakuu hawatahudhuria Mkutano huu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Rais wa Urusi Vladimir Putin na Xi Jinping wa China, wahusika wawili wakuu katika mgogoro wa Syria na Korea Kaskazini, hawatakuwepo katika vikao hivyo.

Nchi za Poland Italia, Hungary na Austria zitawakilishwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

"Tutakabiliwa na hali ngumu," amesema mwanadiplomasia mmoja kutoka nchi ya Kimagharibi ambaye ana imani kuwa diplomasia itakuwa na mchango mkubwa katika hali hii, lakini amesema kuna hatari ya kushindwa kufikia matokeo kuhusu migogoro mikubwa nchini Syria au Yemen.